Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nanyuki Julai 29 walifanya operesheni kali iliyosababisha kupatikana kwa bidhaa kadhaa zinazoshukiwa kuibwa wakati wa maandamano yaliyoshuhudiwa nchini siku chache zilizopita.
Operesheni hiyo iliongozwa na afisa anayesimamia kituo hicho (OCS) na ilifanywa katika kijiji cha Majengo, kaunti ndogo ya Laikipia Mashariki.
Washukiwa walipatikana wakiwa na bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na viatu, nywele, soksi na nyaya za kompyuta.

Huduma ya Taifa ya Polisi inasema washukiwa hao wamewekwa kizuizini wakisubiri kufikishwa mahakamani.