Serikali imezindua sera ya kitaifa ya mwaka 2024 kuhusu watu wanaoishi na ulemavu kuhakikisha usawa, haki na ujumuishaji wa walemavu nchini Kenya.
Katibu katika Idara ya Ulinzi wa Jamii Joseph Motari aliyeongoza uzinduzi huo jijini Nairobi, alitambua jukumu muhimu lililotekelezwa na wapiganiaji wa haki za wanaoishi na ulemavu, hadi kufikia hatua hiyo.
“Sera hii inahusu juhudi zilizopo kama vile kupanua mfumo wa utumaji wa pesa,, kuimarisha mafunzo na kuwapa vifaa vya usaidizi kwa wale walio na mahitaji,” alisema Motari.
Motari alitaja sheria mpya ya watu wanaoishi na ulemavu ya mwaka 2025, kuwa ufanisi mkubwa kwa kuondoa ile ya awali ya mwaka 2003 ambayo aliitaja ilipitwa na wakati na kuimarisha ulinzi wa kisheria na ujumuishaji.
“Lazima tujumuishe sera hii kwa bajeti za kitaifa na za kaunti pamoja na kwenye mikakati ya kazi. Ufanisi unahitaji heshima na kujitolea kwa pamoja,” aliongeza Motari.
Akizungumza katika hafla hiyo, mwanachama wa Tume ya Utumishi wa Umma Harun Hassan, alielezea mafanikio yaliyotekelezwa kama vile kuimarisha ushirikiano wa wadau na mchango kwenye sheri ya walio na ulemavu.