Rais Ruto: Kenya imejitolea kushirikiana na washirika wa kifedha

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akutana na Rais wa Maendeleo ya Benki ya Kiarabu ya kiuchumi Barani Afrika - BADEA

Kenya imepongeza Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika (BADEA), kwa kuendelea kutoa msaada wake kwa miundombinu, afya na kilimo.

Akizungumza alipokutana na Rais wa benki hiyo Abdullah Almusaibeeh katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne, Kiongozi wa taifa alisema Kenya imejitolea kushirikiana na washirika wa kifedha ili kuleta mabadiliko hapa nchini.

“Tumejitolea kushirikiana kwa karibu na washirika wa kifedha, ili kubadilisha taifa hili,” alisema Rais Ruto.

Arab Bank for Economic Development in Africa ni benki ya maendeleo inayomilikiwa na Muungano wa Mataifa ya Kiarabu, ili kutoa ufadhili wa maendeleo kwa nchi za Afrika. Ilianzishwa kulingana na azimio la mkutano wa 6 wa mataifa ya kiarabu huko Algiers mnamo tarehe 28 Novemba mwaka 1973.

Share This Article