Mbunge wa Kajiado Kusini Sakimba Parashina amewataka wenzake katika Bunge la Taifa kutenga fedha zaidi kwenye bajeti ya ziada ijayo ili kusaidia Wizara ya Elimu kutosheleza mahitaji ya kufadhili elimu ya bure ambayo imekuwa gumzo kuuu nchini katika siku za hivi karibuni.
Akizungumza kwenye hafla ya elimu katika eneo bunge lake, Parashina anasema kauli ya Waziri wa Fedha John Mbadi kwamba hamna fedha za kutosha kufadhili elimu nchini ni ya kweli na hivyo wizara hiyo inapaswa kutengewa fedha zaidi ili kuhakiksiah elimu ya bure inaendelea bila kutatizika.
Kwenye hafla hiyo pia ambayo iliandaliwa katika shule ya wasichana ya Kimana, Mbunge huyo aliongoza uzinduzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa chumba cha maakuli, ukarabati wa madarasa pamoja na miradi mingine, akisema kukosekana kwa fedha kumesababisha shule nyingi kuendelea kusalia nyuma katika utekelezaji wa miradi muhimu.