Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel akataa shinikizo la kimataifa la kusitisha vita Gaza

Martin Mwanje
1 Min Read
Gideon Saar - Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar leo Jumanne amekataa kile alichokitaja kuwa “kampeni ya kupotosha” ya shinikizo la kimataifa la kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza na kuitambua Palestina kama taifa. 

Saar aliwaambia wanahabari kuwa ikiwa Israel itasitisha mgogoro huo wakati Hamas bado iko madarakani huko Gaza na bado inawashikilia mateka, hali itakuwa “mbaya zaidi kwa Israel na Palestina”.

“Haitafanyika, haijalishi kiwango cha shinikizo ambacho Israel itawekewa,” alisema Saar.

Israel imekuwa ikifanya operesheni ya kijeshi dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza kwa karibu miezi 22, tangu shambulizi la kuvuka mpaka lililosababisha umwagikaji wa damu lililofanywa na kundi hilo la Palestina Oktoba 7, 2023.

Katika wiki za hivi karibuni, shinikizo la kimataifa limekuwa likiongezeka kwa vita hivyo kusitishwa ili kuruhusu mashirika ya kutoa msaada kuingia Gaza na kusaidia kukabiliana na baa la njaa linalorindima katika eneo hilo.

Lakini akiwahutubia wanahabari mjini Jerusalem, Saar alisisitiza kuwa Hamas ndio inayopaswa kulaumiwa kwa mzozo huo peke yake na kwamba shinikizo dhidi ya Israel litalitia moyo kundi hilo kuchukua msimamo mkali.

“Wakati wanapotaka vita hivi kumalizika, wanamaanisha nini hasa? Kumaliza vita wakati Hamas bado iko madarakani?” alisema Saar.

Share This Article