Wafanyabiashara wakadiria hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa Miwani, Machakos

Martin Mwanje
1 Min Read
Kumeshuhudiwa kizaazaa kwenye barabara ya Kyumbi katika eneo la  Miwani, kaunti ya Machakos baada ya vijana waliojawa na ghadhabu kufuatia kubomolewa kwa vibanda vyao usiku wa kuamkia leo na askari wa kaunti hiyo kufunga barabara hiyo na kuwalazimu maafisa wa polisi kufyatua vitoa machozi kuwatawanya.
Inasemekana usiku wa kuamkia leo, watu wanaokisiwa kuwa maafisa  wa usalama wa kaunti ya Machakos walibomoa vibanda vilivyo kando ya barabara hiyo bila kutoa notisi ya ubomozi kwa wananchi wanaofanyia biashara eneo hilo lililo karibu na barabara ya kuingia katika  afisi ya Gavana wa Machakos eneo la Miwani.
Wananchi sasa wakisalia kukadiria hasara kubwa kubwa kutokana na ubomozi wa usiku na kuwalaumu maafisa wa usalama wa serikali ya kaunti ya Machakos kwa kutekeleza unyama huo.
Baadhi ya tuliozungumza nao wameelezea kupoteza mali zao zenye thamani kubwa na sasa wamesalia bila la kufanya ila kukadiria hasara.
Aidha, serikali ya kaunti ya Mchakos kupitia Waziri  wa Maswala ya Biashara imethibitisha ubomozi huo na kuwataja wafanyabiashara hao kama watu waliokuwa wamevamia ardhi ya umma.
Share This Article