Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen amewasili katika kaunti ya Trans Nzoia tayari kuangazia hali ya usalama katika kaunti hiyo.
Hali hiyo inaangaziwa kupitia mikutano ya Jukwaa la Usalama inayowaleta pamoja maafisa wa serikali ya taifa kuanzia kwa kamishna wa kaunti hadi kwa naibu wa chifu, viongozi wa jamii, wafanyabiashara na vijana.
Kwenye izara hiyo, Murkomen ameandamana na Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Gilbert Masengeli na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jasper Ombati miongoni mwa maafisa wengine wa usalama serikalini.
Waziri huyo amepangiwa kushiriki mkutano kwenye ukumbi wa mji utakaoleta pamoja wakazi na viongozi wa eneo hilo, maafisa wa serikali ya taifa na pia wale wa usalama.