Simba wa Morocco watua Kenya, tayari kwa kipute cha CHAN

Kikosi cha Atlas Lions chenye wachezaji 28 kilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta saa kumi alfajiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Morocco almaarufu Atlas Lions, imekuwa timu ya kwanza kuwasili nchini Kenya mapema leo Jumatatu tayari kushiriki Makala ya nane ya kipute cha CHAN kitakachong’oa nanga Jumamosi hii.

Kikosi cha Atlas Lions chenye wachezaji 28 kilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta saa kumi alfajiri.

Morocco watafungua kampeni ya CHAN Jumapili hii katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo dhidi ya Angola saa tisa alasiri.

Timu nyingine za kundi A, Zambia, itawasili kesho, wakati Angola na DR Congo, zikitarajiwa kutua Alhamisi hii.

Share This Article