Wenyeji Taifa Stars ya Tanzania wamesajili ushindi wa pili wa mabao 2-1, dhidi ya mabingwa watetezi wa CHAN Senegal Jumapili alasiri katika uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mjini Arusha.
Mapathe Mpodi akifungua ukurasa wa magoli kwa Tanzania katika dakika ya nane kabla ya Abdul Hamisi, kusawazisha dakika ya 52 naye Ibrahim Hamad, akahitimisha kibarua kwa bao la ushindi dakika nne baadaye.
Ushindi huo ulikuwa wa pili kwa Tanzania, ambao wameibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuwazabua Uganda Cranes bao moja bila katika mchuano wa ufunguzi.
Senegal pia walikuwa wameshindwa mabao 2-1 na Uganda Cranes.
Timu zote tatu zilitumia mashindano hayo kujiandaa kwa dimba la CHAN kuanzia Jumamosi hii jijini Dares Salaam, wenyeji Tanzania wakikipiga dhidi ya Burkina Faso kundini B.