Vidosho wa Nigeria Super Falcons, walitoka nyuma mabao 2-0 na kuwalemea wenyeji Morocco mabao 3-2, na kutawazwa mabingwa wa Afrika kwa mara ya 10 Jumapili usiku uwanjani Olympique mjini Rabat.
Ghizlane Chebbak na Sanaa Mssoudy waliwaweka kifua mbele wenyeji Morocco ,katika dakika za 12 na 24 mtawalia, Atlas Lionesses wakienda mapumzikoni kwa uongozi wa mabao 2-0.
Esther Okoronkwo alikomboa bao la kwanza kwa Nigeria kunako dakika ya 64, kabla ya Folashade Ijamilusi, kufanya mambo kuwa 2-2 dakika saba baadaye.
Jennifer Echegini alipiga bao la ushindi dakika 2, kabla ya kipenga cha mwisho na kuwapa Super Falcons, kombe la kumi huku Morocco wakimaliza nafasi ya pili kwa mara ya pili mtawalia.
Makala ya mwaka ujao yataandaliwa mwezi Machi mwakani nchini Morocco.