Waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Tusker FC, wamethibitisha kumsajili tena mshambulizi wa zamani Eric Kapaito kutoka Tanzania.
Kapaito aliyetawazwa mfungaji bora misimu miwili katika ligi kuu ya humu nchini kabla ya kuhamia klabu ya Namungo nchini Tanzania bara.
Kapaito aligura Tusker FC mwishoni mwa msimu wa mwaka 2023-24, akifunga mabao 12.
“Tusker FC ndio nyumbani kwangu, nafurahia kurejea, nina uhusiano mkubwa na mashabiki na wachezaji, na nina kiu cha kusajili matokeo mazuri.” akasena Kapaito
Ujio wa mshambuilizi huyo ni wa hivi punde baada ya kutua kwa kiungo Vincent Otieno na beki Eugene Ikutwa waliotokea Nairobi City Stars na Bidco United mtawalia.