Nigeria kukabana koo na wenyeji Morocco, fainali ya WAFCON

Morocco upande wao waliilemea Ghana mabao 4-2, kupitia mikiki ya penati kufuatia sare ya bao moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nigeria maarufu kama Super Falcons, watapambana na wenyeji Morocco, katika fainali ya kuwania kombe la Afrika kwa wanawake maarufu kama WAFCON.

Mabingwa mara tisa Nigeria walifuzu kwa fainali baada ya kuwatimua mabingwa watetezi Afrika Kusini mabao 2-1 katika nusu fainali ya kwanza.

Ajibade Rasheedat alipachika goli la kwanza kupitia penati mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Linda Motlhalo, kusawazishia Afrika Kusini dakika ya 60.

Nigeria walifunga kazi ndani ya dakika 90 baada ya Michelle Alozie kubusu nyavu dakika ya 94.

Morocco upande wao waliilemea Ghana mabao 4-2, kupitia mikiki ya penati kufuatia sare ya bao moja.

Morocco wanaowania tuzo ya kwanza watakumbana na Super Falcons wa Nigeria Jumamosi hii katika fainali.

Afrika Kusini watapimana ubabe na Ghana Ijumaa kwa mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne.

Share This Article