Wakazi wa kaunti ya Busia wametakiwa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti hiyo Catherine Omanyo ambaye anasema hatua hiyo itawaepushia walemavu msongo wa mawazo na kutelekezwa.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Kopiya, eneo bunge la Teso Kaskazini wakati wa kutoa hundi kwa makundi ya kina mama ,vijana na watu wanaoishi na ulemavu, Omanyo amesema kuwa watu wanaoishi na ulemavu wako na vipaji na uwezo mbalimbali kama watu wengine hivyo basi wanahitaji kuungwa mkono katika jamii.
Alitumia fursa huyo kuwasuta wanasiasa wanaoendeleza siasa zisizokuwa na manufaa kwa nchi akidai hawana ajenda yoyote ya kuwanufaisha raia.
Amewataka wakazi wa Busia kuwapuuza wanasiasa kama hao.