Duale apokea ripoti ya ulanguzi wa viungo vya binadamu

Wizara ya Afya inatathmini ripoti hiyo yenye kurasa 313, kabla ya kuandaa mwongozo na ripoti itakayosisitiza kuleta mageuzi mwafaka katika sekta ya upachikaji viungo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Afya Aden Duale leo amepokea ripoti ya kamati hurui ya watu 13 aliyobuni kuchunguza madai ya ulanguzi wa viungo vya binadamu katika hospitali ya Mediheal Eldoret.

Kamati hiyo, ikiongozwa na mtafiti mwandamizi katika taasisi ya utafiti wa kimatibabu nchini KEMRI, Professa Elizabeth Bukusi, ilibuniwa na Duale Aprili 23 mwaka huu, ambapo ilijukumiwa kuwasilisha ripoti ndani ya miezi mitatu.

Wizara ya Afya inatathmini ripoti hiyo yenye kurasa 313, kabla ya kuandaa mwongozo na ripoti itakayosisitiza kuleta mageuzi mwafaka katika sekta ya upachikaji viungo.

Awali, Daule alikatalia mbali ripoti ya awali iliyotolewa mwezi jana.

TAGGED:
Share This Article