Maluki achaguliwa Rais wa kamati ya Olimpiki NOCK

Jumla ya wapiga kura 27 kati ya 29 walishiriki zoezi hilo huku viongozi waliochaguliwa wakitarajiwa kuhudumu kwa miaka minne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shadrack Maluki ndiye Rais mpya wa kamati ya Olimpiki nchini NOC-K, baada ya kuzoa kura 15 kwenye uchaguzi ulioandaliwa leo.

Maluki ambaye amekuwa Naibu Rais wa kwanza amemshinda Katibu Mkuu anayeondoka, Francis Mutuku, kwa kura 12.

Barnaba Korir amechaguliwa Naibu Rais wa kwanza kwa kuzoa kura 15 dhidi ya 12 za mpinzani wake Anthony Ombok Jamal.

Nahashon Randiek ndiye Naibu Rais wa kwanza wakati John Ogola akichaguliwa bila kupingwa kuwa Katibu Mkuu, naye Francis Karugu akachaguliwa Mweka hazina mpya.

Suleiman Sumba, Joyceline Nyambura na Sasha Mutai walichaguliwa wanachama wa kamati kuu.

Viongozi waliochaguliwa watahudumu kwa kipindi cha miaka minne.

Jumla ya wapiga kura 27 kati ya 29 walishiriki zoezi hilo huku viongozi waliochaguliwa wakitarajiwa kuhudumu kwa miaka minne.

 

 

Share This Article