Polisi wapata ng’ombe 145 walioibwa Meru

Martin Mwanje
0 Min Read

Maafisa wa Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS,  katika kaunti ndogo ya Igembe Central, kaunti ya Meru wamepata ng’ombe 145 waliokuwa wameibwa katika eneo hilo.

Ng’ombe hao wamekabidhiwa wenyewe.

“Ng’ombe hao, walioripotiwa kuibwa mapema Julai 20, walipatikana kupitia juhudi zilizoratibiwa za polisi,” ilisema NPS kwenye taarifa.

“Maafisa bado wamepelekwa eneo hilo kuwasaka ng’ombe walioibwa waliosalia huku uchunguzi ukiendelea.”

 

TAGGED:
Share This Article