Wanasiasa wa mrengo wa Gachagua wazuiwa kufanya mkutano Nakuru

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanaisasa wanaogemea mrengo unaoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, walizuiwa kufanya mkutano wa kisiasa waliopanga Jumapili katika eneo la Subukia, kaunti ya Nakuru.

Wakiongozwa na naibu Mwenyekiti wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Cleophas Malala, na Seneta wa Nyandarua, John Methu, hawakuwa na budi ila kusitisha mkutano wao baada ya polisi kufunga barabaraba.

Aidha, polisi walitumia vitoza machozi kuwatawanya wafuasi wao waliokuwa wamekusanyika kwa mkutano huo wa kisiasa.

Baada ya kuhangaishwa mara kadhaa, kundi hilo hatimaye liliwatubia wafuasi wao mjini Nakuru.

Share This Article