Nitatimiza ahadi zangu zote kabla ya mwaka 2027, asema Ruto

Aidha, Rais amekanusha madai ya kutelekeza eneo la Ukambani, akisema atafanya ziara ya kimaendeleo mwezi ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameapa kutimiza ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kabla ya kukamilika kwa muhula wake wa kwanza.

Ruto amesema haya Jumapili katika kanisa la African Inland (AIC) Bomani, kaunti ya Machakos katika hafla ya kusimikwa kwa Askofu Benjamin Kilonzo.

Aidha, Rais amekanusha madai ya kutelekeza eneo la Ukambani, akisema atafanya ziara ya kimaendeleo mwezi ujao.

Pia alitetea utendakazi wa serikali yake akisema imefanikiwa kuwatuma vijana laki nne kufanya kazi ughaibuni tangu atwae mamlaka.

Rais aliandamana na Waziri wa Leba Dkt. Alfred Mutua na viongozi wa Ukambani wakiongozwa na Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti.

Share This Article