Uchaguzi wa kamati ya Olimpiki kuandaliwa Jumatatu ijayo

Uchaguzi wa maafisa wapya ndio ajenda kuu ya mkutano huo mkuu wa mwaka ulioitishwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baada ya kuahirishwa mara mbili, hatimaye uchaguzi wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya, NOC-K, utaandaliwa Jumatatu ijayo Julai 27, jijini Nairobi.

Uchaguzi wa maafisa wapya ndio ajenda kuu ya mkutano huo mkuu wa mwaka ulioitishwa.

Ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuitishwa baada ya kutibuka Aprili 24,baada ya mashirikisho manne kukosa kuafikiana kuhusu wapiga kura wao na kusimamishwa tena tarehe 19 mwezi uliopita na mahakama kuu ya Eldoret.

Kiti cha Urais kina shuhudia ushindano mkali kati ya Naibu Rais wa kwanza, Shadrack Maluki, dhidi ya Katibu mkuu anayeondoka, Francis Mutuku.

Mashirikisho 25, Rais wa sasa Paul Tergat, waakilishi wawili wa wanamichezo na mwakilishi wa wanawake watapiga kura katika uchaguzi wa Jumatatu.

Share This Article