Wakazi wa kaunti ya Trans Nzoia na wanaharakati wa haki za kibinadamu wameionya serikali dhidi kutumia asasi huru za serikali kuwakandamiza viongozi wa upinzani wanaotofautiana na uongozi wa Rais William Ruto kuhusu mustakabali wa nchi.
Wakazi hao wakiongozwa na Paul Wamalwa wanamtaka kiongozi wa taifa kukoma kuzitumia asasi huru za serikali kisiasa hasa kwa kuwanyanyasa na kuwanyamazisha viongozi wanaonekana kutofautiana na serikali ya Kenya Kwanza.
Kulingana nao, hatua ya kuhangaishwa kwa Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya, kufuatia uvamizi uliotekelezwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC nyumbani kwake inazua maswali mengi tata kuhusu uongozi wa nchi.
Kwa sasa, wanataka Gavana Natembeya kupewa mazingira na muda bora wa kuwahudumia wakazi wa kaunti hiyo ili kutimiza ahadi zake kwa manufaa ya ustawi wa kaunti hiyo.