Pombe haramu yanaswa na kuharibiwa Kayole, Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read

Maafisa kutoka kituo cha polisi cha Obama, kaunti ndogo ya Kayole, kaunti ya Nairobi walifanya msako mkali jana Alhamisi katika mtaa wa Kayole ambapo pombe haramu ilinaswa na kuharibiwa.

Operesheni hiyo ilihusisha maafisa kutoka vitengo mbalimbali.

Ililenga maeneo ya kutengeneza pombe haramu katika eneo la Mwengenye karibu na Daraja la Dandora, kando ya Mto Nairobi.

Wakati wa opereshen hiyo, zaidi ya lita 100 ya pombe haramu aina ya kangara na zaidi ya mitungi 10 ya plastiki ya lita 20 inayotumiwa katika uzalishaji wa pombe hiyo iliharibiwa.

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS inasema uchunguzi kwa lengo la kuwakamata watengenezaji wa pombe hiyo unaendelea.

 

Share This Article