Kindumbwendumbwe cha kombe la bara Afrika kwa wanawake, WAFCON kitarejea nchini Morocco kwa mechi za robo fainali.
Mabingwa mara tisa Nigeria watafungua dimba dhidi ya Zambia katika mechi inayotazamiwa kuwa moto wa kuotea mbali kuanzia saa moja usiku katika uwanja wa Larbi Zaouli, mjini Casablanca.
Baadaye, saa nne usiku katika uchanjaa wa Olympique de Rabat, wenyeji Morocco watakabana koo na Mali.
Mechi mbili za awamu ya nane bora zitapigwa kesho Jumamosi, Algeria wakikumbana na Ghana saa moja usiku, huku mabingwa watetezi Afrika Kusini, ukipenda Banyana Banyana, wakimaliza udhia dhidi ya Senegal.