Mshikilizi warekodi ya dunia ya mbio za marathon Ruth Chepng’etich, amepigwa marufuku na kitengo cha maadili ya wanariadha AIU kwa ulaji muku.
Chepng’etich ambaye pia ni bingwa Chicago marathon mara tatu, alipatikana kuwa mtumizi wa dawa iliyoharamishwa ya Hydrochlorothiazide (HCTZ) tarehe 14 mwezi Machi mwaka huu.
Chepng’etich aliye na umri wa miaka 30, alishinda dhahabu ya dunia mwaka 2019,kabla ya kumaliza wa tatu katika mbio za London Marathon mwaka 2020.
Mwanariadha huyo aliandikisha historia kuwa mwanamke wa kwanza kukamilisha mbio za marathon chini ya saa 2 na dakika 10 ,akizitimka kwa saa 2 dakika 9 na sekunde 56.