Wanahabari watakiwa kuwa mabalozi wema wa CHAN

Zaidi ya wanahabari 200 wa michezo kutoka Kenya watawajibika wakati wa michuano ya CHAN itakayopigwa viwanja vya Nyayo na Kasarani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanahabari wa michezo wametakiwa kuwa mabalozi wema wa fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN.

Akizungumza alipokutana na wanahabari wa michezo pamoja na wahariri mapema leo jijini Nairobi, waziri wa michezo Salim Mvurya alisema ufanisi wa mashindano hayo makubwa itategemea mchango wa wanahabari.

Aidha, waziri amesema Kenya iko tayari kuandaa kipute hicjo baada ya kupokonywa miaka ya 1996 na 2018 kwa kukosa viwanja.

Zaidi ya wanahabari 200 wa michezo kutoka Kenya watawajibika wakati wa michuano ya CHAN itakayopigwa viwanja vya Nyayo na Kasarani.

Rais wa shirikisho la soka nchini FKF,Hussein Mohammed, aliyehidhuria kikao hicho aliwataka wanahabari kuwasiliana naye kwa taarifa zozote kuhusu timu ya taifa Harambee Stars wakati wa fainali za CHAN.

 

Share This Article