Makamanda watatu wa jeshi la Syria wauawa katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Syria

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya Reuters

Viongozi watatu wa Syria wameuawa katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Syria, kwa mujibu wa shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria (SOHR).

Kikundi cha kampeni chenye makao yake nchini Uingereza – ambacho hufuatilia na kutoa ripoti kuhusu majeruhi nchini Syria – kinasema kuwa mashambulizi hayo yalilenga misafara ya kijeshi.

Kinasema mashambulizi hayo yalifanyika katika maeneo ya mashambani karibu na vijiji vya Walgha na al-Majimar, karibu na mji wa Suweida ambapo mapigano kati ya makundi yenye silaha ya Druze na Bedouin yametokea katika siku za hivi karibuni.

Awali SOHR iliripoti kwamba maafisa saba wa kijeshi waliuawa katika mashambulizi ya awali ya Israeli huko Suweida, ikiwa ni pamoja na vifaru na magari ya kijeshi kuharibiwa – na kufanya idadi ya waliouawa kufikia angalau 10.

Share This Article