Mrisho Mpoto atangaza kifo cha mke wake

Mwili wa mwendazake kwa jina Mariam, unatarajiwa kuzikwa kesho saa kumi alasiri kwenye makaburi ya familia ya upande wa kwao huko Yombo.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii wa muziki na mashairi nchini Tanzania Mrisho Mpoto ametangaza kifo cha mke wake ambaye alikuwa akiugua.

Mpoto ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutoa habari hizo ambapo alichapisha picha ya mwendazake na kuandika, “NGUMU KUAMINI.. NIMEFIWA NA MKE WANGU”.

Mpoto amefahamisha wanahabari waliowasiliana naye kwamba msiba uko nyumbani kwake katika kata ya kijichi wilaya ya Temeke, eneo la Dar es Salaam.

Mwili wa mwendazake kwa jina Mariam, unatarajiwa kuzikwa kesho saa kumi alasiri kwenye makaburi ya familia ya upande wa kwao huko Yombo.

Kando na mashairi yake Mrisho Mpoto anafahamika kwa mtindo wake wa maisha wa kutembea bila viatu.

Share This Article