Kiambu yafuta bili za hospitali kwa waliojeruhiwa kwenye maandamano

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Afya kaunti ya Kiambu Dkt. Elias Maina.

Serikali ya kaunti ya Kiambu imetangaza kufutiliwa mbali kwa bili za matibabu kwa wale waliojeruhiwa wakati wa maandamano yaliyoshuhudiwa kote nchini.

Waziri wa Afya wa kaunti hiyo Dkt. Elias Maina amesema hatua hiyo iliafikiwa baada ya mashauriano na wadau wakuu katika sekta za afya na huduma za dharura.

Kulingana na Dkt. Maina, hatua hiyo itazipunguzia mzigo wa kifedha familia zilizoathiriwa.

“Tunafahamu kwamba wakazi wetu wengi waliathiriwa kwenye ghasia hizo na kufikishwa katika vituo vyetu vya afya, wengine wakiwa na majeraha mabaya. Kama serikali, tumejitolea kuhakikisha hakuna mkazi atagharimika na bili za hospitali wakati huu mgumu wa kifedha,”alisema Dkt. Maina.

Aidha, aliagiza hospitali zote katika kaunti hiyo kutoa huduma za matibabu kwa wakati na kutowalipisha walioathiriwa.

Share This Article