Mbuzi 15 walioibwa Pokot wapatikana

Mbuzi hao walipelekwa katika kambi ya GSU eneo la Nakwamoru, wakisubiri wamiliki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi kutoka vitengo mbalimbali vya usalama wamepata mbuzi 15 walioibwa katika eneo la Takaiwa, kaunti ndogo ya Pokot Kaskazini, kaunti ya Pokot Magharibi.

Polisi wamesema walianzisha msako punde baada ya kupokea ripoti ya wizi wa mifugo hao na kuafanikiwa kuwapata.

Hata hivyo, wezi hao walitoroka na kuwaacha mbuzi hao katika kijiji cha Kaakali punde baada ya kubaini kuwa walikuwa wanaandamwa na polisi.

Mbuzi hao walipelekwa katika kambi ya GSU eneo la Nakwamoru, wakisubiri wamiliki.

Polisi wangali wanaendelea na msako wa kuwanasa wezi hao wa mifugo.

TAGGED:
Share This Article