Rais Suluhu aongoza kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais Samia Suluhu akiongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 

Kikao hicho ni cha mwisho  cha serikali ya awamu ya sita kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Rais Suluhu analenga kutetea wadhifa huo kupitia chama tawala cha CCM.

Januari 19, CCM iliazimia na kumthibitisha Suluhu kuwa mgombea wake wa urais.

Aidha, kilimteua na kumthibitisha Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa makamu wake.

Hii ni baada ya Makamu wa Rais wa sasa anayeondoka Dkt. Philip Mpango aliomba kupumzishwa wadhifa huo.

Chama cha upinzani cha Chadema kilitarajia mwenyekiti wake Tundu Lissu kuwa mgombea wake ila Lissu amekumbana na visiki vya kila aina katika azima yake ya kumbandua Rais Suluhu madarakani.

Lissu kwa sasa anakabiliwa na mashtaka uhaini, mashtaka ambayo ameyapuuzilia mbali akiyataja kuwa ya kisiasa.

Rais Suluhu anakabiliwa na tuhuma za kuwakandamiza wapinzani ili awe na mtihani rahisi wa kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

 

Share This Article