Kocha Odero, afariki katika ajali ya barabarani

Odero alikuwa kocha wa leseni ya CAF B, na alishika hatamu za kuinoa Fortune Sacco, Aprili mwaka huu kufuatia kujiuzulu Michael Etimong.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha mkuu wa klabu ya Fortune Sacco FC, Sylvester Odero, amefariki mapema leo katika ajali ya barabarani eneo la Mwea, kaunti ya Kirinyaga.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, gari la marehemu Odero, lilipoteza mwelekeo kubingiria mara kadhaa, kabla ya kutumbukia kwenye mto Kanaro.

Kando na kuwa mkufunzi wa Fortune Sacco FC, Odero, pia alikuwa mwalimu katika shule ya sekondari ya Nyaikungu, na yamkini alikuwa safarini kuelekea shuleni wakati wa ajali.

Odero alikuwa kocha wa leseni ya CAF B, na alishika hatamu za kuinoa Fortune Sacco, Aprili mwaka huu kufuatia kujiuzulu Michael Etimong.

Fortune Sacco FC hushiriki ligi ya daraja ya kwanza nchini NSL.

Share This Article