Rais wa Cameroon, mwenye umri wa miaka 92, kugombea tena urais

Martin Mwanje
1 Min Read
Paul Biya - Rais wa Cameroon

Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 92 ametangaza kuwa atagombea uchaguzi wa urais utakaoandaliwa Oktoba 12 mwaka huu.

Biya ambaye anatafuta kuhudumu kwa muhula wa nane, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka 43 iliyopita, alitoa tangazo hilo jana Jumapili usiku kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia tangazo hilo, Biya ambaye ni kiongozi mzee zaidi duniani kote alielezea dhamira yake ya kuendelea kuliongoza taifa hilo kukabiliana na kile alichokitaja kuwa “nyakati ngumu.”

“Nawahakikishia kuwa dhamira yangu ya kuhudumu inawiana na dharura ya changamoto zinazotukabili,” Biya alisema alisema kwenye tangazo hilo.

Rais amekuwa madarakani tangu mwaka wa 1982 na kufanya Rais mkongwe zaidi ambaye yupo madarakani duniani kote.

Katiba ya nchi hiyo ilifanyiwa marekebisho ili kuondoa ukomo wa mihula ya kuhudumu ya Rais.

Katika nchi jirani ya Uganda, Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80, pia ametangaza kuwa atatetea kiti chake kwenye uchaguzi wa urais katika hatua itakayorefusha uongozi wake wa takriban miaka 40 madarakani.

Museveni aliingia madarakani mnamo mwaka wa 1986.

Uchaguzi umepangwa kufanyika nchini Uganda mapema mwakani.

Share This Article