Harambee Stars waingia siku ya pili kambini kujiandaa kwa CHAN

Kikosi hicho kinajiandaa kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye kipute cha CHAN, ambacho hushirikisha wacheza wa ligi za nyumbani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wachezaji wa timu ya taifa ya Harambee Stars, wameingia siku ya pili ya kambi ya mazoezi uwanjani Kasarani,kujiandaa kwa fainali za nane za Kombe la CHAN kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

Kikosi hicho kinajiandaa kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye kipute cha CHAN, ambacho hushirikisha wacheza wa ligi za nyumbani.

Chini yabukufunzi wa kocha Benni McCarthy, Harambee Stars watafungua dimba tarehe 3 mwezi ujao katika uwanja wa Kasarani, dhidi ya Chui kutoka Congo waliotwaa kombe hilo mara mbili.

Timu nyingine kundini A pamoja na Kenya ni Morocco, Angola na Zambia.

Fainali hizo zitakazoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania zitashirikisha mataifa 19 kwa nara ya kwanza Disemba mwaka huu.

Share This Article