Rais William Ruto, ameahidi kuwa serikali yake itawachukulia hatua za kisheria wote waliohusika katika ufujaji wa pesa za vyama vya ushirika nchini, ikiwemo kuwashurutisha kuzirejesha na kutumikia kifungo.
Kwenye hotuba yake iliyosomwa na Waziri mwenye mamlaka Musalia Mudavadi katika sherehe za 103 za maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika nchini maarufu Ushirika Day,zilizoadhimishwa katika ukumbi wa KICC siku ya Jumamosi.
Aidha, Ruto amepongeza mchango maridhawa wa vyama vya ushirika nchini katika ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake, Waziri wa vyama vya ushirika na mashirika madogo na ya kadri ya kibiashara Wycliff Oparanya, amesema sekta hiyo inatarajiwa kunufaika pakubwa punde muswada wa mwaka 2024, wa vyama ushirika utapitiswa na bunge la Seneti.