Rais Ruto kuongoza upanzi wa miti Elgeyo Marakwet

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto kuongoza upanzi wa miti katika msitu wa kaptagat.

Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza Makala ya tisa ya shughuli ya kutunza msitu wa Kaptagat huko Kapchorwa, kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Akizungumza huko Kapchorwa  waziri wa mazingira na misitu Deborah Barasa alitoa wito kwa wakenya kuunga mkono azma ya rais ya kupanda miche alfu 15 ifikiapo mwka wa 2032.

Waziri Barasa alikariri umuhimu wa sheria ya kusimamamia misitu katika kulinda raslimali za kiasili. Alisema asilimia 90 ya msitu huo imerejeshwa na hivyo kusaidia kuimarisha maisha ya wakazi.

Barasa piaalimpongeza katibu wa hazina ya kitaifa Chris Kiptoo, ambaye ni madhamini wa mpango huo kwa juhudi zake za kuhifadhi msitu huo na kuwataka wakenya zaidi kukumbatia mpango huo.

Mkuu wa utumishi wa umma Dkt. Felix Koskeialisema eneo hilo limerejesha asilimia 36 ya eneo lake la misitu na hivyo kufaidi wakazi.

Shughuli hiyo imepangw akufuatia wito wa mkuu wa utumishi wa umma kwamba mashirika ya serikali yahusike kwente juhudi za upanzi wa miti.

Miongoni mwa mashirika yaliyokumbatia wito huo ni shirika la utangazaji nchini KBC. Rais Ruto anatarajiw akuongoza hafla hiyo.

Share This Article