Mbunge wa Manyatta John Mukunji ameachiliwa kwa dhamana ya shilimgi laki tatu pesa taslimu, baada ya kufikishwa kwa Mahakama ya Kahawa kaunti ya Kiambu.
Mukunji na washukiwa wengine wawili John Mbochi ambaye ni mwanahabari na mhudumu wa boda boda Stanely Mbuthi, walikamatwa wakati wa maandamano ya saba saba Julai 7,202, kwa madai ya kuchochea vurugu.
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), iliwasilisha maombi mahakamani ikitaka watatu hao wazuiliwe kwa siku 14 zaidi, ili iweze kukamilisha uchunguzi.
Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali ombi hilo na kuwapa dhamana.Upande wa mashtaka ulidai watatu hao walikuwa wakichunguzwa kwa makosa yanayohusiana na ugaidi.