Wanaopanga machafuko wakati wa maandamano wataadhibiwa, asema Murkomen

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa Taifa  Kipchumba Murkomen, amesisitiza kwamba maandamano yaliyoshuhudiwa hivi majuzi na ambayo yalisababisha maafa na uharibifu wa mali, yalipangwa na watu aliowataja kuwa wakuu wa machafuko.

Murkomen alisema serikali itachukua hatua kali dhidi ya watu aliowataja kuwa wanaopanga kupindua serikali, huku akitoa wito kwa wananchi kujiepusha na visa vya kuwashambulia maafisa wa polisi.

Akizungumza kwenye kaunti ya Tana River, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kaunti ndogo ya  Tarasaa, waziri huyo alitoa wito kwa jamii mbali mbali kuishi kwa amani na utangamano na maafisa wa polisi.

Waziri alisema bunduki mbili zilizoibwa kati ya bunduki tano katika kituo cha polisi cha Dagoretti tayari zimepatikana.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mrakibu wa eneo la Pwani Rhoda Onyancha, Seneta wa Tana River Danson Mungatana, mbunge wa Garsen na Kamanda wa Polisi eneo la Pwani Ali Nuno miongoni mwa wengine.

Share This Article