Rais wa zamani wa Korea Kusini akamatwa tena

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa zamani wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol aliyekamatwa tena timu maalum ya waendesha mashtaka

Rais wa zamani wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol amekamatwa tena leo Alhamisi na timu maalum ya waendesha mashtaka wa nchi hiyo.

Yoon alikamatwa kwa tuhuma za kuzuia majukumu maalum ya serikali na makosa mengine yanayohusiana na tangazo lake lililodumu kwa muda mfupi la sheria ya kijeshi mwezi Disemba mwaka jana.

Rais huyo wa zamani alikamatwa na kushtakiwa mwezi Januari kwa makosa ya uhaini.

Aliachiliwa huru mwezi Machi mwaka huu.

Kesi ya uhalifu dhidi yake kwa sasa inaendelea.

Mawakili maalum waliteuliwa na kuanzisha uchunguzi huru usiohusiana na serikali baada ya Rais Lee Jae-myung kuingia madarakani mwezi Juni mwaka huu.

Timu hiyo iliomba kibali cha kumkamata Yoon Julai 6, ikidai kuwa aliagiza idara ya usalama wa Rais izuie kukamatwa kwake mwezi Januari.

 

Share This Article