Hatima ya Makamishna wa IEBC kubainika Alhamisi

Jaji Lawrence Mugambi aliruhusu  kuendelea kwa usaili wa Makamishna hao, ila akazuia uapisho wao hadi kesi itakapoamuliwa.

Dismas Otuke
1 Min Read
Erastus Ethekon Edung, Mwenyekiti wa IEBC

Hatima ya Makamishna saba wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, inatarajiwa kubainika leo Alhamisi wakati jopo la majaji watatu litatoa uamuzi kuhusu kesi iliyowasilishwa kupinga uteuzi huo.

Saba hao waliteuliwa na Rais William Ruto mwezi Juni mwaka huu.

Kesi hiyo iliyowasilishwa na Kelvin Roy Omondi na mwanaharakati  Boniface Mwangi,  inapinga uteuzi wa makamishna hao kwa misingi kwamba  ulikiuka sheria, ulikosa ushirikishwaji wa umma na pia unakosa usawa wa kimaeneo pamoja na kukosa ufaafu kwa baadhi ya Makamishna walioteuliwa.

Jaji Lawrence Mugambi aliruhusu  kuendelea kwa usaili wa Makamishna hao ila akazuia uapisho wao hadi kesi itakapoamuliwa.

Jopo la majaji hao linalojumuisha Mugambi, John Chigiti, na  Roselyne Aburili linatarajwia kutoa uamuzi majira ya saa nane adhuhuri leo Alhamisi, uamuzi ambao utabaini hatima ya IEBC kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 20227.

Share This Article