2024 WAFCON: Morocco, Zambia wanusia robo fainali

Morocco wanaongoza kundi A kwa alama 4 sawia na Zambia wakifuatwa Senegal kwa alama 3 huku DR Congo wakishika nanga pasi na alama.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Morocco na Zambia walijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali ya kipute cha Kombe la Afrika kwa wanawake baada ya kushinda mechi zao za pili jana Jumatano usiku.

Morocco walikuwa na kibarua kigumu kabla ya kuwabwaga Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) mabao 4-2.
Katika mchuano mwingine wa kundi hilo, Zambia walikuwa na wakati mgumu kabla ya kuwanyuka Senegal magoli 3-2.

 

Morocco wanaongoza kundi A kwa alama 4 sawia na Zambia wakifuatwa Senegal kwa alama 3 huku DRC wakishika nanga pasi na alama.

Tunisia watamenyana na Algeria leo katika kundi B saa moja usiku, wakati mabingwa mara 9 Super Falcons kutoka Nigera wakipimana nguvu na Botswana saa nne usiku.

Mechi zote mbili zitarushwa mubashara na runinga ya KBC Channel 1.

Share This Article