Serikali imejiandaa vyema kukabiliana na wanaosababisha na kuchochea ghasia nchini, katika juhudi za kulinda mali ya Wakenya na haki za kidemokrasia.
Haya yalisemwa jana jioni Rais William Ruto, alipokutana na viongozi wa chama cha United Democratic Movement (UDM), katika Ikulu ya Nairobi.
Aidha Ruto alikariri kuwa kamwe watu wachache hawataruhusiwa kubatilisha uamuzi wa Wakenya, na uongozi wa nchi kwa njia za kinyemela.
Viongozi wa UDM waliokuwa Ikuluni waliongozwa na kinara wa chama hicho Ali Roba.