Rais William Ruto amesifia ushirikiano wa dhati wa miaka 60 ambao umekuwepo kati ya Kenya na Japani.
Kwa kipindi hicho, Ruto anasema Japani imetekeleza wajibu muhimu katika kuchochea maendeleo ya miundombinu humu nchini, ikiwa ni pamoja na katika sekta za elimu, ICT na nishati kijani miongoni mwa zingine.
Hususan, Rais Ruto aliishukuru Japani kwa kuchangia maendeleo ya nchi hii kupitia mpangokazi wa Mkutano wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Afrika wa Tokyo (TICAD).
Kiongozi wa nchi aliyasema hayo alipokutana na Rais wa TICAD Akihiko Tanaka katika Ikulu ya Nairobi.