Seneti yasikiliza hoja ya Gavana Guyo wa Isiolo kuondolewa mamlakani

Tom Mathinji
1 Min Read
Amason Kingi - Spika wa Bunge la Seneti

Bunge la Seneti limeanza vikao vya siku mbili leo Jumanne, kusikiliza hoja ya kuondolewa mamlakani kwa Gavana wa kaunti ya Isiolo Abdi Ibrahim Guyo.

Spika wa Seneti Amason Kingi alichapisha vikao hivyo kwenye gazeti rasmi la serikali, ikizingatiwa kuwa bunge hilo kwa sasa liko kwenye mapumziko mafupi.

Kulingana na Spika Kingi, hoja hiyo itasikilizwa na bunge lote, baada ya pendekezo la kubuniwa kwa kamati teule kukataliwa mbali.

Guyo anakabiliwa na makosa ya ukiukaji wa katiba na sheria zingine, utumizi mbaya wa mamlaka na utovu wa maadili.

Iwapo atapatikana na kosa moja kati ya hayo, basi atapoteza wadhifa wa kuhudumu kama Gavana wa Isiolo.

Share This Article