Waziri wa Polisi Afrika Kusini adaiwa kushirikiana na wahalifu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa polisi nchini Afrika Kusini Senzo Mchunu.

Waziri wa polisi nchini Afrika Kusini Senzo Mchunu,  amedaiwa kushirikiana na magenge ya wahalifu huku akidaiwa kuingilia uchunguzi wa polisi kuhusu mauaji yaliyochochewa kisiasa.

Madai haya yalitolewa na Mkuu wa Polisi wa KwaZulu-Natal Nhlanhla Mkhwanazi, katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili.

Alisema Bw Mchunu alikuwa akipokea usaidizi wa kifedha kutoka kwa mfanyabiashara anayedaiwa kuwa fisadi ili kufadhili “juhudi zake za kisiasa”.

Bw Mchunu tangu wakati huo amekanusha kile anachosema ni “madai ya kipumbavu” huku Rais Cyril Ramaphosa akisema “yanatia wasi wasi mkubwa wa usalama wa taifa” na “yanapewa kipaumbele cha juu zaidi”.

Jenerali Mkhwanazi alielezea kwa kina mlolongo wa matukio anayodai yalisababisha kuvunjwa kwa jopo kazi lililoundwa mwaka wa 2018 kuchunguza mauaji ya wanasiasa, hususan KwaZulu-Natal.

TAGGED:
Share This Article