Banyanabanyana kuanza kutetea kombe la WAFCON, dhidi ya Ghana leo

Kipute hicho kitakachokamilika Julai 26, kinachoendelea nchini Morocco,kinashirikisha mataifa 12.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Afrika Kusini almaarufu Banyanabanyana, wataanza kampeni ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu kwa wanawake dhidi ya Black Starlets kutoka Ghana.

Mchuano huo wa kundi C utang’oa nanga saa moja usiku, kabla ya Twiga Stars kutoka Tanzania, kuhitimisha mechi za mzunguko wa kwanza dhidi ya Mali kuanzia saa nne usiku.

Mechi zote zitarushwa mubashara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.

Kipute hicho kitakachokamilika Julai 26, kinachoendelea nchini Morocco,kinashirikisha mataifa 12.

Share This Article