Spika Wetang’ula akariri umuhimu wa umoja wa kitaifa

Wetang'ula amesema ipo haja ya viongozi wa kisiasa mifano bora iliyoachwa na viongozi kama vile Ronald Ngala na Masinde Muliro .

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, amekariri umuhimu wa umoja wa kitaifa huku akikashifu saisa za ukabila.

Akizungumza huko Msambweni kaunti ya Kwale, siku ya Jumapili katika hafla ya kuazindua miradi ya maendeleo ,Wetang’ula  alionya kuwa siasa za ukabila huenda zikagawanya taifa vibaya.

Wetang’ula amesema ipo haja ya viongozi wa kisiasa mifano bora iliyoachwa na viongozi kama vile Ronald Ngala na Masinde Muliro .

Viongozi kadhaa waliozungumza pia wamewaonya vijana dhidi ya kutumiwa na wanasiasa  kupitia siasa  za migawanyiko.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni kiranja wa wengi bungeni Syvannus Osoro,mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ngeno ,mbunge wa Nandi Hill Benard Kitur ,Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir ,Gavana wa Kilifi Fatma Achani na mawaziri Hassan Joho na  Salim  Mvurya.

Share This Article