Klabu ya Liverpool imetangaza kuwa itaendelea kulipa mshahara wa pauni 140,000, kwa kila wiki kwa familia ya mshambulizi Digo Jota, aliyefariki kwenye ajali ya barabarani mapema wiki hii.
Liverpool italipa mshahara huo kwa mkewe kwa kipindi cha miaka miwili iliyosalia kwenye mktaba wa marehemu Jota.
Haya yametangazwa Jumamosi na uongozi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Uingereza, wakati wa mazishi ya Jota, eneo la Gondomar, nchini Ureno.

Jota aliye na umri wa miaka 28 aliaga dunia akiwa na kakake mdogo kwenye ajali ya barabarani nchini Uhispania wakati gari lao lilipopasuka gurudumu na kushika moto.