KNEC yazindua mtandao wa kuthibitisha vyeti vya mitihani

Aidha, Bitok amesema Wizara imeanzisha miongozo ya mitandaoni kwa walimu wa elimu ya mtaala mpya wa umilisi (CBC).

Dismas Otuke
1 Min Read

Baraza la kitaifa la mitihani nchini KNEC, limezindua mtambo wa kidijitali wa kuthibitisha vyeti ghushi na halali.

Katibu wa elimu ya msingi Julius Bitok amesema mtambo huo ambao utakuwa ukitumia APP, utawekwa katika afisi za idara ya huduma za utumishi ili kuharakisha kuthibitisha na kubainisha vyeti halali na ghushi.

Hii inafuatia hatua ya tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC kuanzisha msako wa kitaifa kukabiliana na wafanyikazi wenye vyeti ghushi.

Kesi kadhaa ziko mahakamani kuhusu washukiwa wenye vyeti bandia.

Aidha, Bitok amesema Wizara imeanzisha miongozo ya mitandaoni kwa walimu wa elimu ya mtaala mpya wa umilisi (CBC).

Bitok alikuwa akisema haya Jana Ijumaa katika makao makuu ya KNEC, alipoongoza ufunguzi wa kituo cha kutoa miongozo ya walimu kinacholenga kuinua viwango na ubora wa mafunzo nya walimu .

Kituo hicho kinafadhiliwa na serikali ,wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza na afisi ya maendeleo ya Jumuiya ya Madola.

TAGGED:
Share This Article