Rais Ruto: Kanisa jipya lajegwa Ikulu ya Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amethibitisha kuwa kanisa jipya linajengwa katika Ikulu ya Nairobi.

Akizungumza alipokutana na viongozi wa mashinani wa kaunti ya Embu katika Ikulu ya Nairobi, kiongozi wa taifa alisema fedha za umma hazitumiki katika ujenzi huo, kwa kuwa unatekelezwa na fedha zake binafsi.

“Naambiwa kwa magazeti leo wanasema najenga kanisa State House, ni ukweli. I have no apologies to make for that. Hapa State House nilikuta kanisa ya mabati. Na sijengi na pesa ya serikali, najenga na pesa yangu.”

Kanisa katika Ikulu ya Nairobi.

Rais alidokeza kuwa, alipochukua hatamu za uongozi alipata kanisa moja ambalo limejengwa kwa mabati lililokuwa likitumika kwa ibada, ambalo sasa anataka kuliboresha.

Aliwahakikishia viongozi hao kwamba serikali imejitolea kutekeleza miradi ya maendeleo kote nchini.

TAGGED:
Share This Article