Majaribio ya kitaifa ya mashindano ya Riadha Duniani yataandaliwa Julai 22 katika uwanja wa Ulinzi Complex .
Mashindano hayo yamerudishwa nyuma kutoka tarehe ya awali ya Agosti 1 na 2 kutokana na uwanja wa Ulinzi ambao utakuwa na shughuli nyingine.
Wanariadha watakaoshiriki ni wale tu watakaoalikwa baada ya kutimiza muda wa kufuzu na masharti ya shirika la maadili ya wanariadha AIU.
Kenya italenga kuteua kikosi dhabiti kwa makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan, kati ya Septemba 13 na 121 mwaka huu.
Kenya inapania kuboresha matokeo ya mwaka 2023 mjini Budapest, Hungary, ilipomaliza ya tano kwa jumla ya medali 3 za dhahabu 3 na shaba 4.