Kocha wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Benni McCarthy, ametangaza kikosi cha awali kitakachoshiriki fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani almaarufu CHAN.
Baadhi ya wachezaji kikosini ni wafungaji bora katika Ligi Kuu Moses Shuma, Emmanuel Osoro na Ryan Ogam.
Kiungo cha kati kinasheheni Mohammed Bajaber wa Police FC , Keith Imbali,Yakeen Muteheli na Staphod Odhiambo.
Kikosi hicho kimeratibiwa kuripoti kambini Julai 10, kwa mazoezi kujiandaa kwa kipute cha CHAN.
Harambee Stars itafungua mechi za CHAN kundini A, dhidi ya mabingwa mara mbili DR Congo Agosti 3 ugani Kasarani.
Timu nyingine kundini A pamoja na Kenya ni Zambia,mabingwa mara mbili Morocco na Angola.
Kikosi kamili
Makipa
Faruk Shikhalo (Bandari), Sebastian Wekesa (Kariobangi Sharks), Brian Opondo (Tusker FC)
Mabeki
Siraj Mohammed (Bandari FC), Manzur Suleiman (KCB), Pamba Swaleh (Bandari FC), Abud Omar (Kenya Police),Alphonce Omija (Gor Mahia), Sylvester Owino (Gor Mahia), Michael Kibwage (Tusker), Daniel Sakari (Kenya Police), Lewis Bandi (AFC Leopards), Kevin Okumu (KCB)
Viungo
Brian Musa( Kenya Police), Kelly Madada (AFC Leopards), Keith Imbali (Shabana), Alpha Onyango (Gor Mahia), Mathias Isogoli (KCB), Staphod Odhiambo (Ulinzi Stars), Austine Odhiambo (Gor Mahia), Ben Stanley (Gor Mahia)
Washambulizi
Mohammed Bajaber (Kenya Police), Boniface Muchiri (Ulinzi Stars), David Sakwa (Bandari), Emmanuel Osoro (FC Talanta), Yakeen Muteheli (Ulinzi Stars), Edward Omondi (Sofapaka), Ryan Ogam (Tusker),Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Beja Nyamawi (Bandari)